Nafasi za Kazi za Mkataba Wilaya ya Tunduru 2026
Hili hapa tangazo rasmi la ajira mpya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, chini ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), linalohusu nafasi za kazi za Mkataba kwa wananchi wa Tanzania wenye sifa stahiki.
Taarifa za Jumla za Tangazo:
- Mwajiri: Halamashauri ya Wilaya ya Tunduru
- Idara: Usafi wa Mazingira
- Aina ya Ajira: Mkataba
- Idadi ya Nafasi: Nafasi 06
- Tarehe ya Tangazo: 13 Januari 2026
- Kumb. Na: TDC.L.40/31/53
Ajira Mpya Zilizotangazwa
Wazoaji Taka – Nafasi 06
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hizi anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na afya njema
- Awe mwenye akili timamu
- Awe na uwezo wa kusoma na kuandika
- Awe na bidii ya kazi pamoja na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi bila kusimamiwa
- Awe na nidhamu na uaminifu
- Awe ni mtu mwenye uwezo wa kushirikiana na wengine
- Awe tayari kufanya kazi za usafi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kama atakavyo pangiwa na mwajiri
- Awe na kitambulisho kimoja wapo kati ya:
- Kitambulisho cha Uraia (NIDA)
- Mpiga Kura
- Asiwe mtumishi wa umma kwa ngazi yoyote ile
Kazi na Majukumu ya Mwombaji
- Kupakia taka kwenye gari
- Kufanya kazi ya usafi katika maeneo atakayopangiwa na mwajiri wake
Malipo kwa Mwezi
- Kibarua cha Kupakia Taka: Tshs 170,000 kwa mwezi
- Kibarua cha Kufagia: Tshs 160,000 kwa mwezi
Nyaraka za Kuambatanisha
Waombaji wote wanatakiwa kuambatanisha nakala zifuatazo:
- Nakala ya Kitambulisho cha NIDA au Mpiga Kura
- Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yaandikwe na kuwasilishwa kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
S.L.P 2/5
Tunduru – Ruvuma
Mwisho wa Kutuma Maombi
19 Januari 2026
Saa 9:30 Alasiri
Soma zaidi:
Tags: Tunduru