Nafasi za Kazi NECTA
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi (ajira) kutoka Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania, maarufu kama NECTA, ni taasisi ya serikali inayohusika na usimamizi wa mitihani ya taifa nchini Tanzania. NECTA ina jukumu la kuhakikisha mitihani inafanyika kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa, kwa kuzingatia haki, usawa, na ubora wa elimu.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| S/N | Jina La Tangazo | Idadi Ya Nafasi | Jina La Mwajiri |
|---|---|---|---|
| 1 | Msaidizi Wa Uchapishaji Daraja La Pili | Nafasi 5 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 2 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Utalii Na Ukarimu) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 3 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Utekelezaji Wa Muziki) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 4 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Sanaa Ya Uchoraji) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 5 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Sanaa Za Maonyesho) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 6 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Elimu Ya Michezo Na Mazoezi Ya Mwili) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 7 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Sayansi Ya Uchumi Wa Nyumbani) | Nafasi 2 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 8 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Sayansi Ya Kilimo) | Nafasi 2 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 9 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Sayansi Ya Kompyuta) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
| 10 | Afisa Mitihani Daraja La Pili (Huduma Na Mauzo Ya Chakula Na Vinywaji) | Nafasi 1 | Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) |
Jinsi ya Kutuma maombi
Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
Secretary,
Presidents Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.
Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.
Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.
Tags: NECTA