Nafasi za Kazi za Mkataba Wilaya ya Tunduru 2026

Filed in Ajira by on January 13, 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo rasmi la ajira mpya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, chini ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), linalohusu nafasi za kazi za Mkataba kwa wananchi wa Tanzania wenye sifa stahiki.

Taarifa za Jumla za Tangazo:

  • Mwajiri: Halamashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Idara: Usafi wa Mazingira
  • Aina ya Ajira: Mkataba
  • Idadi ya Nafasi: Nafasi 06
  • Tarehe ya Tangazo: 13 Januari 2026
  • Kumb. Na: TDC.L.40/31/53

Ajira Mpya Zilizotangazwa

Wazoaji Taka – Nafasi 06

Sifa za Mwombaji

Mwombaji wa nafasi hizi anatakiwa awe na sifa zifuatazo:

  1. Awe raia wa Tanzania
  2. Awe na afya njema
  3. Awe mwenye akili timamu
  4. Awe na uwezo wa kusoma na kuandika
  5. Awe na bidii ya kazi pamoja na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi bila kusimamiwa
  6. Awe na nidhamu na uaminifu
  7. Awe ni mtu mwenye uwezo wa kushirikiana na wengine
  8. Awe tayari kufanya kazi za usafi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kama atakavyo pangiwa na mwajiri
  9. Awe na kitambulisho kimoja wapo kati ya:
    • Kitambulisho cha Uraia (NIDA)
    • Mpiga Kura
  10. Asiwe mtumishi wa umma kwa ngazi yoyote ile

Kazi na Majukumu ya Mwombaji

  1. Kupakia taka kwenye gari
  2. Kufanya kazi ya usafi katika maeneo atakayopangiwa na mwajiri wake

Malipo kwa Mwezi

  • Kibarua cha Kupakia Taka: Tshs 170,000 kwa mwezi
  • Kibarua cha Kufagia: Tshs 160,000 kwa mwezi

Nyaraka za Kuambatanisha

Waombaji wote wanatakiwa kuambatanisha nakala zifuatazo:

  • Nakala ya Kitambulisho cha NIDA au Mpiga Kura
  • Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yaandikwe na kuwasilishwa kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
S.L.P 2/5
Tunduru – Ruvuma

Mwisho wa Kutuma Maombi

19 Januari 2026
Saa 9:30 Alasiri

Soma zaidi:

Tags:

Comments are closed.