Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs 2026

Filed in Ajira by on January 8, 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs 2026 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya taasisi mbalimbali za Serikali anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba ajira kuwa usaili unatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 18 Januari 2026 hadi 14 Februari 2026.

Baada ya usaili, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi kulingana na kada walizoomba.

Taasisi Zinazohusika na Usaili Huu

Usaili huu unahusisha waombaji wa ajira kutoka taasisi zifuatazo:

  • Wizara, Taasisi za Serikali (MDAs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs)

Bonyeza hapa kudownload PDF

Muda na Mahali pa Usaili

  • Muda wa Usaili: 18/01/2026 – 14/02/2026
  • Muda na Mahali: Umeainishwa kwa kila Kada kulingana na tangazo rasmi

Muhimu: Msailiwa ahakikishe anasoma tangazo lake kwa makini ili kujua tarehe, muda na eneo sahihi.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa Wote

Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

Mahudhurio ya Usaili

  • Msailiwa afike kwa tarehe, muda na eneo lililopangwa kwa kada yake.

Barakoa (Mask)

  • Kila msailiwa anatakiwa kuvaa barakoa wakati wote wa usaili.

Kitambulisho cha Utambulisho

Msailiwa lazima awe na kitambulisho halisi. Vitambulisho vinavyokubalika ni:

  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kitambulisho cha Kazi
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Hati ya Kusafiria (Passport)
  • Leseni ya Udereva
  • Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji

Nyaraka Muhimu za Kuja Nazo

Msailiwa anatakiwa kufika na vyeti vyake halisi, vikiwemo:

  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
  • Cheti cha Kidato cha Sita (Form VI)
  • Astashahada / Stashahada
  • Stashahada ya Juu
  • Shahada au zaidi (kulingana na kada)

Muhimu Sana:
Nyaraka zifuatazo HAZITAKUBALIWA:

  • Testimonials
  • Provisional Results
  • Statement of Results
  • Result Slips za Form IV na Form VI

Msailiwa atakayewasilisha nyaraka hizo HATARUHUSIWA kuendelea na usaili.

Usajili wa Bodi za Kitaaluma

Kwa kada zinazohitaji usajili:

  • Lete cheti halisi cha usajili
  • Lete leseni halisi ya kufanyia kazi

Mavazi na Gharama

  • Msailiwa atajigharamia mwenyewe chakula, usafiri na malazi
  • Mavazi yawe:
    • Nadhifu
    • Yenye staha
    • Yanayozingatia Waraka wa Mavazi Serikalini

Wasailiwa Waliosoma Nje ya Tanzania

  • Vyeti lazima viwe vimehakikiwa na kuidhinishwa na:
    • TCU
    • NACTVET
    • NECTA
  • Kada zinazohitaji GPA:
    • Wasilisha cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU

Hujaona Jina Lako Kwenye Tangazo?

  • Ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal
  • Angalia sababu za kutokuitwa
    Hii itakusaidia kurekebisha mapungufu kwa fursa zijazo.

Namba ya Usaili na Akaunti ya Ajira Portal

  • Nakili Namba yako ya Usaili
  • Kwa usaili wa mtandaoni:
    • Kumbuka barua pepe (email)
    • Kumbuka nywila (password) ya Ajira Portal

Tofauti ya Majina Kwenye Nyaraka

  • Wasailiwa wenye majina yanayotofautiana:
    • Wasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll)
    • Iwe imesajiliwa Wizara ya Ardhi

Ushauri wa Mwisho:
Hakikisha unajiandaa mapema, unakuwa na nyaraka zote halisi, na unafuata maelekezo yote ili kuepuka kunyimwa fursa ya usaili.

Soma zaidi:

Tags:

Comments are closed.