Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Biolojia (Biology) 2026
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Nafasi 332 za Ualimu wa Kujitolea 2026 – OWM-TAMISEMI (Mradi wa GPE-TSP) Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Biolojia (Biology) 2026.
Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) kupitia Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu (Global Partnership for Education – Teacher Support Programme, GPE-TSP) inatekeleza afua mbalimbali za kuimarisha ubora wa elimu nchini. Miongoni mwa afua hizo ni kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea katika Shule za Sekondari zilizo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kupitia mradi huu, OWM-TAMISEMI inatangaza nafasi 332 za Ualimu wa Kujitolea kwa Shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa, kwa kuzingatia Utaratibu wa Upangaji wa Walimu wa Shule za Sekondari (Secondary Teacher Allocation Protocol – S-TAP).
Wigo wa Nafasi Zinazotangazwa
Nafasi hizi zinalenga walimu wenye sifa katika maeneo yafuatayo:
- Sayansi na Teknolojia (STEM)
- Masomo ya Amali (Vocational Subjects)
- Masomo ya Biashara (Business Studies)
Watanzania wenye sifa wanakaribishwa kuwasilisha maombi ya nafasi hizi 332 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.
Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Biolojia
- Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Biolojia kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali; au
- Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biolojia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali; au
- Stashahada ya Ualimu yenye somo la kufundishia la Biolojia kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
Soma zaidi:
- Nafasi za Kazi za Mkataba Wilaya ya Tunduru 2026
- Nafasi za Kazi NAOT 2026
- Walioitwa Kwenye Usaili NHC 2026
- Walioitwa Kwenye Usaili NOAT 2026
- Walioitwa Kwenye Usaili CAMARTEC 2026
- Nafasi 1,500 za Ualimu wa Kujitolea TAMISEMI 2026
- Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Kemia (Chemistry) 2026
- Walioitwa Kwenye Usaili VETA 2026
Tags: Mwalimu