Kuitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2026

Filed in Ajira by on February 9, 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Leo tarehe 09 Februari, 2026, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana wote walioomba Ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Uhamiaji kutembelea akaunti zao za maombi ya ajira kupitia tovuti ya Uhamiaji https://www.immigration.go.tz na kwa barua pepe zao ili kupokea taarifa na maelekezo ya tarehe na eneo la kufanya usaili kwa waliochaguliwa.

Wasailiwa wote wanatakiwa kuwa na namba ya ombi la Ajira (Application ID) kama ilivyotumwa kwenye akaunti na barua pepe ya mwombaji, Kitambulisho chenye picha yake (Mfano, Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Kitambulisho chochote kinachomtambulisha kwa sasa) pamoja na Kalamu ya wino wa bluu.

Kwa wasailiwa wenye fani za TEHAMA, udereva na ufundi magari wajiandae kwa usaili wa vitendo (Practical Examination). Aidha, Wasailiwa wote watatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili. Kwa changamoto/maulizo wasilisha kupitia: ajira@immigration.go.tz.

Limetolewa na;
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
09 Februari, 2026

Soma zaidi:

Tags:

Comments are closed.