Tag: Uhamiaji
Kuitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2026
Leo tarehe 09 Februari, 2026, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana wote walioomba Ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Uhamiaji kutembelea akaunti zao za maombi ya ajira kupitia tovuti ya Uhamiaji https://www.immigration.go.tz na kwa barua pepe zao ili kupokea taarifa na maelekezo ya tarehe na eneo la kufanya usaili kwa waliochaguliwa.
Wasailiwa wote wanatakiwa kuwa na namba ya ombi la Ajira (Application ID) kama ilivyotumwa kwenye akaunti na barua pepe ya mwombaji, Kitambulisho chenye picha yake (Mfano, Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Kitambulisho chochote kinachomtambulisha kwa sasa) pamoja na Kalamu ya wino wa bluu.
Kwa wasailiwa wenye fani za TEHAMA, udereva na ufundi magari wajiandae kwa usaili wa vitendo (Practical Examination). Aidha, Wasailiwa wote watatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili. Kwa changamoto/maulizo wasilisha kupitia: ajira@immigration.go.tz.
Limetolewa na;
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
09 Februari, 2026
Soma zaidi:
Nafasi za Kazi Idara ya Uhamiaji Zanzibar 2026
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi au ajira mpya kutoka Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Idara ya Uhamiaji Tanzania anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa waombaji wa Zanzibar wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Nne (04), kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Mhasibu Daraja la II – Nafasi 3
2. Msaidizi wa Hesabu Daraja la II – Nafasi 1
Jinsi ya Kutuma maombi Uhamiaji
Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.
Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.
Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.zanajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.
Soma zaidi”
- Nafasi za Kazi Wilaya ya Handeni 2026
- Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025
- Fursa 500 za Ajira kwa Madereva Pikipiki UAE (2026)
- Nafasi za Kazi Wilaya ya Songwe 2025
- Nafasi za Kazi Shirika la ndege Air Tanzania 2025
- Nafasi za Kazi UDOM 2025
- Walioitwa Kazini Ajira Portal 2026
- Malipo ya Kujitolea Serikalini 2026
- Mwongozo wa Kujitolea Serikalini 2026
- Mwongozo wa Kujitolea Katika Utumishi wa Umma 2026
- Nafasi za Kazi Wilaya ya Gairo 2026
Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025
Tangazo Rasmi la Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025 hadi Januari 2026 Maombi yatume kupitia mfumo wa ajira e-recruitment.immigration.go.tz.
Tangazo hili limetolewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa mujibu wa Kifungu Na. 11(1) cha Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, likitangaza nafasi za Ajira Mpya za Konstebo wa Uhamiaji kwa vijana wa Kitanzania.
Muhtasari wa Haraka:
- Mwajiri: Idara ya Uhamiaji Tanzania
- Nafasi: Konstebo wa Uhamiaji
- Kuanza Maombi: 29 Desemba 2025
- Mwisho wa Maombi: 11 Januari 2026
- Tovuti ya Maombi: https://e-recruitment.immigration.go.tz
- Mahali pa Kazi: Tanzania nzima
Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote ya Serikali
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa
- Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho kutoka NIDA
- Awe na siha njema ya mwili na akili
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya
- Asiwe na rekodi ya uhalifu au jinai
- Asiwe na tatoo/choro mwilini
- Awe hajaoa/hajaolewa wala kuwa na mtoto
- Umri na Elimu:
- Kidato cha Nne: Miaka 18–22, Daraja I–III
- Astashahada/Stashahada: Miaka 18–25
- Shahada/Stashahada ya Juu: Miaka 18–30
- Awe tayari kupata mafunzo ya awali ya Kijeshi ya Uhamiaji
- Awe tayari kufanya kazi popote Tanzania
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za mchakato wa ajira
Maombi Yatakayopata Kipaumbele
Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji wenye Shahada, Stashahada au Astashahada kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:
- Lugha za Kimataifa
- Utawala
- Sheria
- Uhasiano
- TEHAMA:
- Cyber Security
- Database Developer
- System Developer
- Artificial Intelligence & Machine Learning
- Masijala
- Ukatibu Mahsusi
- Uhasibu
- Ununuzi na Ugavi (waliosajiliwa na Bodi)
- Takwimu
- Uchumi
- Umeme
- Ufundi wa AC
- Brass Band
- Saikolojia (Psychology)
- Mpiga Chapa (Printer)
Kipaumbele cha Ziada:
- Ufundi wa Magari
- Udereva
Namna ya Kufanya Maombi
Maombi yote ya ajira yawasilishwe mtandaoni pekee kupitia: https://www.immigration.go.tz
Soma zaidi:
- Fursa 500 za Ajira kwa Madereva Pikipiki UAE (2026)
- Nafasi za kazi NACTVET 2025
- Nafasi za Kazi TIE 2025
- Nafasi za Kazi TAA 2025
- Nafasi za Kazi IAA 2025
- Nafasi za Kazi NECTA
- Nafasi za Kazi Wilaya ya Songwe 2025
Dirisha la Maombi:
- Kuanza: 29 Desemba 2025
- Mwisho: 11 Januari 2026
Nyaraka za Kuambatisha (PDF – ≤300Kb kila moja)
- Picha ya Pasipoti (jpg/png ≤300Kb)
- Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
- Barua ya utambulisho:
- Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia
- Kwa walioko JKT/JKU: Barua kutoka Makao Makuu ya Kambi
- Cheti cha Kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA
- Index Numbers za Kidato cha Nne na Sita
- Namba ya Utambuzi wa Cheti (TCU/NACTVET) kwa Astashahada, Stashahada au Shahada ya Juu
Tahadhari Muhimu:
- Maombi yatapokelewa kupitia mfumo rasmi pekee
- Nyaraka za kughushi zitapelekea hatua za kisheria
- Epuka matapeli wanaodai fedha au rushwa kwa ahadi za ajira
Mawasiliano
Barua Pepe: ajira@immigration.go.tz
Imetolewa na:
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji
Uzunguni, Dodoma
S. L. P. 1181
04 Barabara ya Mwangosi