Mafunzo kwa Wafanyakazi wa ndani ya Ndege Air Tanzania

Filed in Ajira by on January 29, 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Shirika la Ndege la Tanzania ATCL limetangaza nafasi za mafunzo kwa Wafanyakazi wa ndani ya Ndege (Cabin Crew) ambapo mafunzo hayo yatatolewa kupitia kituo cha Shirika hilo kilichopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam.

Kituo cha Mafunzo cha ATCL kinafuraha kutangaza ufunguzi wa maombi ya kozi yake ya wafanyakazi ndani ya ndege (Cabin Crew). Kozi hii ya miezi mitatu (3) imepangwa kuanza tarehe 9 Machi, 2026.

Shirika la Ndege la Tanzania ATCL
Shirika la Ndege la Tanzania ATCL

Sifa za Mwombaji

Umri: Kuanzia miaka 18 hadi miaka 25.

Michoro mwilini: Mwombaji asiwe na michoro ya kudumu mwilini (tattoos).

Muonekano: Awe mwenye akili timamu na mwenye urefu wa kuanzia futi 5’4 (162cm).

Elimu: Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne na ufaulu angalau wa masomo manne kwa alama “D”. Somo la Kiingereza na Jiografia ni lazima.

Lugha: Awe na uwezo wa kuongea na kuandika kwa ufasaha Kiswahili na Kiingereza. Aidha, mwombaji mwenye uelewa wa lugha nyingine zaidi ya kigeni kama Kiarabu, Kichina au Kifaransa atapewa kipaumbele.

Uraia: Awe Mtanzania au raia wa kigeni mwenye vibali halali vinavyomruhusu kusoma nchini. Waombaji kutoka nchi za kigeni wanatakiwa kuwasilisha matokeo ya vyeti vyao Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ili kupata ulinganifu wa matokeo.

Barua ya Maombi

Maombi yote ni lazima yaambatanishwe na nyaraka zifuatazo:

  • Nakala ya cheti cha kidato cha nne na vyeti vingine vya shule/chuo alichohitimu.
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Picha mbili ndogo (passport size) na picha moja yenye kuonyesha umbo lote ukubwa wa 6×8.
  • Wasifu wa mwombaji (Curriculum Vitae – CV).

Kuwasilisha Maombi

Maombi yawasilishwe kwa Mkuu wa Chuo, Jengo la Chuo cha ATCL (Ofisi ya Utawala), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal One au kupitia barua pepe:

training@airtanzania.co.tz

Maombi yote yatumiwe kabla ya tarehe 15 Februari, 2026.

Anuani:

  • Mkuu wa Chuo,
  • ATCL Training Center,
  • S.L.P 543, Dar es Salaam.

Mawasiliano:

  • Piga: +255 754 345 874
  • Au: +255 690 787 568

Soma zaidi:

Tags: ,

Comments are closed.