Nafasi za Kazi Wilaya ya Kilolo 8
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuomba nafasi (08) za kazi baada ya kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao.
Ajira Mpya zilizotangazwa Kilolo
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 8
Soma zaidi:
- Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Biolojia (Biology) 2026
- Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Kemia (Chemistry) 2026
- Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Fizikia (Physics)
- Nafasi 1,500 za Ualimu wa Kujitolea TAMISEMI 2026
Jinsi ya Kutuma maombi Handeni
Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Kilolo,
S.L.P. 2324,
KILOLO.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22 Januari, 2026.
Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.
Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.
Rejea:
Tags: Kilolo