Nafasi za Kazi Wilaya ya Ludewa 2025
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi au ajira mpya Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa anawatangazia watanzania wenye sifa za kuomba nafasi za kazi nane (8) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:-
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
| S/N | Jina La Tangazo | Idadi Ya Nafasi | Jina La Mwajiri | Tarehe Ya Mwisho |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Dereva Daraja La Pili | Nafasi 4 | Halmashauri Ya Wilaya Ya Ludewa | 11/01/2026 |
| 2 | Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Pili | Nafasi 4 | Halmashauri Ya Wilaya Ya Ludewa | 11/01/2026 |
Pitia zaidi:
Jinsi ya Kutuma maombi TLSB
Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,
S.L.P 19,
LUDEWA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.
Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.
Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.
Soma zaidi”
Tags: Ludewa