Nafasi za Kazi Wilaya ya Songwe 2025

Filed in Ajira by on December 29, 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi tano (5) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao: –

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

1. Dereva Daraja la II – Nafasi 5

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Soma zaidi:

Jinsi ya Kutuma maombi Songwe

Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili na ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Songwe
S.L.P 77,
SONGWE

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06 Januari, 2026.

Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.

Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.

Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).

Bonyeza hapa kudownload PDF

Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.

Tags:

Comments are closed.