Fursa 500 za Ajira kwa Madereva Pikipiki UAE (2026)
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Tangazo la Fursa 500 za Ajira kwa Madereva Pikipiki UAE (2026) maombi yatumwe kwenye mfumo wa
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kushirikiana na kampuni ya Target Tours and Labour Supply Company Limited, inawatangazia Watanzania wenye sifa stahiki kutuma maombi ya ajira ya Madereva wa Pikipiki ili kujaza nafasi 500 zilizoidhinishwa na kampuni ya Velo Logistics Delivery Services LLC ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Maelezo ya Fursa ya Ajira
| Kigezo | Maelezo |
|---|---|
| Nafasi ya Ajira | Dereva wa Pikipiki |
| Taasisi | Velo Logistics Delivery Services LLC |
| Nchi | Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) |
| Idadi ya Nafasi | 500 |
| Umri | Miaka 20 hadi 37 |
Soma zaidi:
- Nafasi za kazi NACTVET 2025
- Nafasi za Kazi TIE 2025
- Nafasi za Kazi TAA 2025
- Nafasi za Kazi IAA 2025
- Nafasi za Kazi NECTA
- Nafasi za Kazi Wilaya ya Songwe 2025
Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe na elimu ya msingi au sekondari
- Awe na leseni halali ya udereva wa pikipiki
- Awe na uzoefu wa kazi wa angalau miaka 2 katika udereva wa pikipiki
- Awe na hati ya kusafiria (Passport)
- Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiingereza
- Awe mwanamume
Masharti na Manufaa ya Ajira
- Mshahara utalipwa kwa kuzingatia Sheria za Kazi za UAE
- Gharama za matibabu kwa kipindi chote cha ajira zitagharamiwa na mwajiri
- Tiketi ya kwenda na kurudi itagharamiwa na mwajiri
- Malazi na chakula vitagharamiwa na mwajiri katika miezi miwili (2) ya mwanzo wa ajira
- Mwajiri atalipia gharama zote za usafiri wa kutoka nyumbani hadi kituo cha kazi katika miezi miwili ya mwanzo
Aina ya Ajira
- Mkataba wa ajira wa miaka miwili, unaoweza kuhuishwa
Daraja la Leseni
- Daraja A, A1 au A3
Ratiba ya Usaili
Dar es Salaam
19, 20 na 21 Januari, 2026
Lumumba, Kariakoo – Jengo la Tahmeed (Ghorofa ya 2)
Mwanza
22, 23 na 24 Januari, 2026
Jengo la Exim Bank (Ghorofa ya 3)
Tanga
26, 27 na 28 Januari, 2026
Jengo la Anjuman
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wanatakiwa:
- Kutuma Wasifu (CV) zao kupitia:
- https://www.targettours.co.tz
- info@targettours.co.tz
- +255 784 989 905 / +255 766 712 222 / +255 764 375 757
- Baada ya kutuma maombi, kujisajili kwenye mfumo wa ajira wa Serikali kupitia: https://jobs.kazi.go.tz