Ajira Mpya 1,500 za Ualimu wa Kujitolea TAMISEMI 2026

Filed in Ajira by on January 14, 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Ajira Mpya 1,500 za Ualimu wa Kujitolea 2026 – OWM-TAMISEMI (Mradi wa GPE-TSP) walimu wa sekondari kada ya walimu.

Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) kupitia Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu (Global Partnership for Education – Teacher Support Programme, GPE-TSP) inatekeleza afua mbalimbali za kuimarisha ubora wa elimu nchini. Miongoni mwa afua hizo ni kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea katika Shule za Sekondari zilizo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kupitia mradi huu, OWM-TAMISEMI inatangaza nafasi 1,500 za Ualimu wa Kujitolea kwa Shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa, kwa kuzingatia Utaratibu wa Upangaji wa Walimu wa Shule za Sekondari (Secondary Teacher Allocation Protocol – S-TAP).

Wigo wa Nafasi Zinazotangazwa

Nafasi hizi zinalenga walimu wenye sifa katika maeneo yafuatayo:

  • Sayansi na Teknolojia (STEM)
  • Masomo ya Amali (Vocational Subjects)
  • Masomo ya Biashara (Business Studies)

Watanzania wenye sifa wanakaribishwa kuwasilisha maombi ya nafasi hizi elfu moja na mia tano (1,500) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

Majukumu ya Jumla ya Mwalimu wa Kujitolea

Mwalimu wa Kujitolea atawajibika kutekeleza majukumu yafuatayo kwa mujibu wa miongozo ya elimu:

  1. Maandalizi ya Kitaaluma
    • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
  2. Zana za Ufundishaji na Ujifunzaji
    • Kutengeneza na kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia kwa kuzingatia mitaala husika.
  3. Ufundishaji na Tathmini
    • Kufundisha, kufanya tathmini za wanafunzi na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya kitaaluma.
  4. Usimamizi wa Mahudhurio
    • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani.
  5. Malezi na Ustawi wa Wanafunzi
    • Kusimamia malezi ya wanafunzi kiakili, kimwili na kiroho, pamoja na kutoa ushauri nasaha na unasihi.
  6. Ushauri wa Kitaalamu
    • Kutoa ushauri wa kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya elimu shuleni.
  7. Usimamizi wa Mali za Shule
    • Kusimamia na kutunza vifaa na mali za shule kwa uadilifu na uwajibikaji.
  8. Majukumu Mengine ya Shule
    • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na mahitaji na majukumu ya shule.

Bonyeza hapa kupakua PDF

Soma zaidi:

Tags:

Comments are closed.