Nafasi za Kazi TAA 2025
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi (ajira) Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA), ni wakala wa serikali unaohusika na usimamizi, uendeshaji, na maendeleo ya viwanja vya ndege vinavyomilikiwa na serikali nchini Tanzania. TAA inalenga kuhakikisha usafiri wa anga unakuwa salama, wenye ufanisi, na unaochangia maendeleo ya uchumi na jamii.
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
| S/N | Jina La Tangazo | Idadi Ya Nafasi | Jina La Mwajiri |
|---|---|---|---|
| 1 | Msimamizi Wa Kuongoza Ndege Uwanjani Daraja La Pili | Nafasi 23 | Mamlaka Ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) |
| 2 | Msaidizi Wa Uchapishaji Daraja La Pili (Uhandisi Wa Mitambo) | Nafasi 1 | Taasisi Ya Elimu Tanzania (TIE) |
| 3 | Msaidizi Wa Uchapishaji Daraja La Pili (Uhandisi Wa Umeme) | Nafasi 1 | Taasisi Ya Elimu Tanzania (TIE) |
| 4 | Msaidizi Wa Uchapishaji Daraja La Pili (Sanaa Ya Michoro Na Teknolojia Ya Uchapishaji) | Nafasi 2 | Taasisi Ya Elimu Tanzania (TIE) |
Jinsi ya Kutuma maombi IAA
Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
Secretary,
Presidents Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.
Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.
Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.
Soma zaidi:
Tags: TAA