Nafasi za kazi TLSB 2025
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi au ajira mpya kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), ni taasisi ya serikali inayohusika na maendeleo, usimamizi, na uendeshaji wa huduma za maktaba nchini Tanzania.
TLSB inalenga kukuza utamaduni wa kusoma, kujifunza, na kupata taarifa sahihi kwa maendeleo ya elimu, jamii, na taifa kwa ujumla.
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
| S/N | Jina La Tangazo | Idadi Ya Nafasi | Jina La Mwajiri |
|---|---|---|---|
| 1 | Mkutubi Daraja La Pili | Nafasi 13 | Bodi Ya Huduma Za Maktaba Tanzania (TLSB) |
| 2 | Msaidizi Wa Maktaba Daraja La Pili | Nafasi 7 | Bodi Ya Huduma Za Maktaba Tanzania (TLSB) |
| 3 | Mkufunzi Daraja La Pili (Usimamizi Wa Kumbukumbu Na Nyaraka) | Nafasi 1 | Bodi Ya Huduma Za Maktaba Tanzania (TLSB) |
| 4 | Mkufunzi Daraja La Pili (Usimamizi Wa Maktaba Na Taarifa) | Nafasi 1 | Bodi Ya Huduma Za Maktaba Tanzania (TLSB) |
Soma zaidi:
Jinsi ya Kutuma maombi TLSB
Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
Secretary,
Presidents Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.
Waombaji watakaoteuliwa katika orodha ya awali (shortlist) pekee ndio watakaopata taarifa kuhusu tarehe ya usaili.
Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa zisizo za kweli utachukuliwa kama kosa la kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mhusika.
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
http://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya PSRS kwa kubofya sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine yoyote tofauti na mfumo uliobainishwa hayatazingatiwa.
Tags: TLSB