Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025

Filed in Ajira by on December 29, 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Tangazo Rasmi la Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025 hadi Januari 2026 Maombi yatume kupitia mfumo wa ajira e-recruitment.immigration.go.tz.

Tangazo hili limetolewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa mujibu wa Kifungu Na. 11(1) cha Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, likitangaza nafasi za Ajira Mpya za Konstebo wa Uhamiaji kwa vijana wa Kitanzania.

Muhtasari wa Haraka:

  • Mwajiri: Idara ya Uhamiaji Tanzania
  • Nafasi: Konstebo wa Uhamiaji
  • Kuanza Maombi: 29 Desemba 2025
  • Mwisho wa Maombi: 11 Januari 2026
  • Tovuti ya Maombi: https://e-recruitment.immigration.go.tz
  • Mahali pa Kazi: Tanzania nzima

Sifa za Mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Awe Raia wa Tanzania
  2. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote ya Serikali
  3. Awe na Cheti cha Kuzaliwa
  4. Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho kutoka NIDA
  5. Awe na siha njema ya mwili na akili
  6. Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya
  7. Asiwe na rekodi ya uhalifu au jinai
  8. Asiwe na tatoo/choro mwilini
  9. Awe hajaoa/hajaolewa wala kuwa na mtoto
  10. Umri na Elimu:
  • Kidato cha Nne: Miaka 18–22, Daraja I–III
  • Astashahada/Stashahada: Miaka 18–25
  • Shahada/Stashahada ya Juu: Miaka 18–30
  1. Awe tayari kupata mafunzo ya awali ya Kijeshi ya Uhamiaji
  2. Awe tayari kufanya kazi popote Tanzania
  3. Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za mchakato wa ajira

Maombi Yatakayopata Kipaumbele

Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji wenye Shahada, Stashahada au Astashahada kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:

  • Lugha za Kimataifa
  • Utawala
  • Sheria
  • Uhasiano
  • TEHAMA:
    • Cyber Security
    • Database Developer
    • System Developer
    • Artificial Intelligence & Machine Learning
  • Masijala
  • Ukatibu Mahsusi
  • Uhasibu
  • Ununuzi na Ugavi (waliosajiliwa na Bodi)
  • Takwimu
  • Uchumi
  • Umeme
  • Ufundi wa AC
  • Brass Band
  • Saikolojia (Psychology)
  • Mpiga Chapa (Printer)

Kipaumbele cha Ziada:

  • Ufundi wa Magari
  • Udereva

Namna ya Kufanya Maombi

Maombi yote ya ajira yawasilishwe mtandaoni pekee kupitia: https://www.immigration.go.tz

Soma zaidi:

Dirisha la Maombi:

  • Kuanza: 29 Desemba 2025
  • Mwisho: 11 Januari 2026

Nyaraka za Kuambatisha (PDF – ≤300Kb kila moja)

  • Picha ya Pasipoti (jpg/png ≤300Kb)
  • Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
  • Barua ya utambulisho:
    • Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia
    • Kwa walioko JKT/JKU: Barua kutoka Makao Makuu ya Kambi
  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA
  • Index Numbers za Kidato cha Nne na Sita
  • Namba ya Utambuzi wa Cheti (TCU/NACTVET) kwa Astashahada, Stashahada au Shahada ya Juu

Tahadhari Muhimu:

  • Maombi yatapokelewa kupitia mfumo rasmi pekee
  • Nyaraka za kughushi zitapelekea hatua za kisheria
  • Epuka matapeli wanaodai fedha au rushwa kwa ahadi za ajira

Mawasiliano

Barua Pepe: ajira@immigration.go.tz

Imetolewa na:

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji
Uzunguni, Dodoma
S. L. P. 1181
04 Barabara ya Mwangosi

Tags:

Comments are closed.