Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025
Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.
Tangazo Rasmi la Ajira za Konstebo wa Uhamiaji – Desemba 2025 hadi Januari 2026 Maombi yatume kupitia mfumo wa ajira e-recruitment.immigration.go.tz.
Tangazo hili limetolewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa mujibu wa Kifungu Na. 11(1) cha Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, likitangaza nafasi za Ajira Mpya za Konstebo wa Uhamiaji kwa vijana wa Kitanzania.
Muhtasari wa Haraka:
- Mwajiri: Idara ya Uhamiaji Tanzania
- Nafasi: Konstebo wa Uhamiaji
- Kuanza Maombi: 29 Desemba 2025
- Mwisho wa Maombi: 11 Januari 2026
- Tovuti ya Maombi: https://e-recruitment.immigration.go.tz
- Mahali pa Kazi: Tanzania nzima
Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote ya Serikali
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa
- Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho kutoka NIDA
- Awe na siha njema ya mwili na akili
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya
- Asiwe na rekodi ya uhalifu au jinai
- Asiwe na tatoo/choro mwilini
- Awe hajaoa/hajaolewa wala kuwa na mtoto
- Umri na Elimu:
- Kidato cha Nne: Miaka 18–22, Daraja I–III
- Astashahada/Stashahada: Miaka 18–25
- Shahada/Stashahada ya Juu: Miaka 18–30
- Awe tayari kupata mafunzo ya awali ya Kijeshi ya Uhamiaji
- Awe tayari kufanya kazi popote Tanzania
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za mchakato wa ajira
Maombi Yatakayopata Kipaumbele
Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji wenye Shahada, Stashahada au Astashahada kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:
- Lugha za Kimataifa
- Utawala
- Sheria
- Uhasiano
- TEHAMA:
- Cyber Security
- Database Developer
- System Developer
- Artificial Intelligence & Machine Learning
- Masijala
- Ukatibu Mahsusi
- Uhasibu
- Ununuzi na Ugavi (waliosajiliwa na Bodi)
- Takwimu
- Uchumi
- Umeme
- Ufundi wa AC
- Brass Band
- Saikolojia (Psychology)
- Mpiga Chapa (Printer)
Kipaumbele cha Ziada:
- Ufundi wa Magari
- Udereva
Namna ya Kufanya Maombi
Maombi yote ya ajira yawasilishwe mtandaoni pekee kupitia: https://www.immigration.go.tz
Soma zaidi:
- Fursa 500 za Ajira kwa Madereva Pikipiki UAE (2026)
- Nafasi za kazi NACTVET 2025
- Nafasi za Kazi TIE 2025
- Nafasi za Kazi TAA 2025
- Nafasi za Kazi IAA 2025
- Nafasi za Kazi NECTA
- Nafasi za Kazi Wilaya ya Songwe 2025
Dirisha la Maombi:
- Kuanza: 29 Desemba 2025
- Mwisho: 11 Januari 2026
Nyaraka za Kuambatisha (PDF – ≤300Kb kila moja)
- Picha ya Pasipoti (jpg/png ≤300Kb)
- Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
- Barua ya utambulisho:
- Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia
- Kwa walioko JKT/JKU: Barua kutoka Makao Makuu ya Kambi
- Cheti cha Kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA
- Index Numbers za Kidato cha Nne na Sita
- Namba ya Utambuzi wa Cheti (TCU/NACTVET) kwa Astashahada, Stashahada au Shahada ya Juu
Tahadhari Muhimu:
- Maombi yatapokelewa kupitia mfumo rasmi pekee
- Nyaraka za kughushi zitapelekea hatua za kisheria
- Epuka matapeli wanaodai fedha au rushwa kwa ahadi za ajira
Mawasiliano
Barua Pepe: ajira@immigration.go.tz
Imetolewa na:
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji
Uzunguni, Dodoma
S. L. P. 1181
04 Barabara ya Mwangosi
Tags: Uhamiaji