Nafasi za Kujiunga na Jeshi JKT 2026

Filed in Ajira by on January 20, 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Nafasi za Kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kwa kujitolea mwaka 2026

Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yanawatangazia Vijana wote wa Kitanzania Bara na Visiwani kuhusu fursa za kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea kwa mwaka 2026.

Tangazo hili limetolewa na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, kwa lengo la kuwahamasisha vijana wenye sifa mbalimbali kuchangamkia nafasi hizi muhimu za uzalendo na maendeleo binafsi.

Utaratibu wa Kuomba

Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kujitolea unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi.

Vijana wanashauriwa kuwasiliana na ofisi hizo kwa maelekezo ya kina kuhusu namna ya kuwasilisha maombi yao.

Fani na Taaluma Zinazohitajika

Kipaumbele kitatolewa kwa vijana wenye sifa zifuatazo:

Ngazi ya Diploma

  • Diploma in Information Technology
  • Diploma in Business Information Systems
  • Diploma in Computer Science
  • Diploma in Information and Communication Technology (ICT)
  • Diploma in Cyber Security and Digital Forensics

Ngazi ya Shahada (Bachelor Degree)

  • Bachelor of Science in Computer Science
  • Bachelor of Science in Information Technology
  • Bachelor of Science in Computer Engineering
  • Bachelor of Science in Business Information Technology
  • Bachelor of Science in Cyber Security and Digital Forensics
  • Bachelor of Science in Computer Networks and Information Security Engineering

Aidha, vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali wanahimizwa pia kutuma maombi kupitia Mikoa yao.

Ratiba ya Usaili na Mafunzo

  • Usaili wa vijana wanaoomba kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kujitolea utaanza tarehe 26 Januari 2026 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
  • Vijana watakaofaulu usaili watatakiwa kuripoti Makambi ya JKT kuanzia tarehe 27 Februari 2026 hadi 04 Machi 2026.

Fursa Baada ya Mafunzo

Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuwatangazia vijana kuwa:

  • Mafunzo ya JKT hayatoi ajira ya moja kwa moja,
  • Hata hivyo, hutoa msingi muhimu wa kujiajiri,
  • Husaidia kupata fursa za ajira katika Asasi za Ulinzi na Usalama, Mashirika ya Serikali, pamoja na Sekta binafsi,
  • Mafunzo haya huwajengea vijana nidhamu, uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kushiriki katika shughuli za kujenga na kulinda Taifa.

Taarifa Zaidi

Sifa kamili za mwombaji pamoja na maelekezo ya kina yanapatikana kwenye Tovuti rasmi ya JKT www.jkt.mil.tz

Bonyeza hapa kudownload PDF

Hitimisho

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, anawahimiza vijana wote wanaokidhi vigezo kujitokeza kwa wingi kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea ili kujenga uzalendo, umoja wa kitaifa na kuchangia maendeleo ya Taifa letu.

Soma zaidi:

Tags:

Comments are closed.